Bab Kubwa

Ndugu wana ukumbi naomba tujadili hili suala la ku'cheat' (kudanganya) kwenye mapenzi, yupi ana 'cheat' zaidi kati ya wanaume na wanawake? najuwa mwanamme atasema mwanamke ana 'cheat' zaidi na mwanamke vile vile atasema mwanamme ndio ana 'cheat' zaidi, lakini la muhimu ni kuangalia vigezo na ushahidi katika hilo.

Uwanja uko wazi kutoa maoni yako katika suala hili.

Share

Reply to This

Replies to This Discussion

Waaohh!! Nimeipenda sana hii maada maana imenigusa mnoo!! Kutokana na uchunguzi wangu nimegundua wanawake wanadanganya zaidi!! Kwasababu wanawake wengi huwa hawariziki na maisha waliyonayo,hapa namaanisha kuwa huwa wanatamaa ya kutaka kupata zaidi hivyo utakuta mwanamke ana mpenzi wake anayempa senti lakini bado atatafuta wa pembeni mwenye senti zaidi,labda kisa shoga yake ana bwana mwenye hela kuliko wake!! So atakuwa na wapembeni kisa anapata hela zaidi. Jamani wanawake mbadilike maradhi ni mengi na UKIMWI upo mrudieni Mungu.

Reply to This

ni vizuri tungejua uongo wa aina hani maana naweza kumuachia mia mbili akienda sokoni anabania nkirudi ananambia kuwa ela imeisha nao ni uongo huo ama kwenye mapenzi
mwanaume anacheat pale amtakapo mwanamke lakini akishampata haoni sababu ya kumcheat sipokuwa kama ni mtu asiyerizika, ama mwanake atakudanganya hapo mwanzo hata akiwa ndani,

Reply to This

Na kwa nini umdanganye mwanammke siku ya mwanzo unapomtaka kwani utakapomueleza ukweli nini kitatokezea au unahofia nini? mimi sioni sababu ya kudanganya. na kama umesema mwanamke atakudanganya hapo mwanzo hata akiwa ndani basi ni same thing na mwanamme ikiwa atakudanganya hapo mwanzo basi aweza kukudanganya hata akisha kukuweka ndani kwani ajuwa tayari amekwisha kukumiliki na huwezi kutoka kirahisi.

raul said:
ni vizuri tungejua uongo wa aina hani maana naweza kumuachia mia mbili akienda sokoni anabania nkirudi ananambia kuwa ela imeisha nao ni uongo huo ama kwenye mapenzi
mwanaume anacheat pale amtakapo mwanamke lakini akishampata haoni sababu ya kumcheat sipokuwa kama ni mtu asiyerizika, ama mwanake atakudanganya hapo mwanzo hata akiwa ndani,

Reply to This

Mwanamke ni soo dah! mimi nasema hv coz nauzoefu i tinc tuwe macho kwa ujumla hasa we mans kwa kweli2nadanganywa sana ila 2navumilia sana katika familia zetu

Reply to This

Kwanza nijenge hoja kisha baadae nitoe maoni yangu,nikizingatia udanganyifu kati ya mme na mke huenda niizame sana upande wa mapenzi ila nikazama kwenye udanganyifu kwa ujumla.



Moja,Adam mtu wa kwanza hakuwa na mpango kabisa wa kula tunda la nyoka pale bustanini lakini Hawa mama yetu wa kwanza anajua mwenyewe jinsi alivyomperemba mmewe mpaka akakubali,Hawa alidanganywa na Shetani yeye nae akaubeba ule udanganyifu hadi kwa Adam na Adam akaingia kingi.



Pili,Ninavuta picha hadi kwa Rebeka mke wa Isaka naweza kumuona akiumia kichwa kwamba afanyeje ili ampige changa la macho mumewe ili ambariki Yakobo badala ya Esau, na ninaweza kuona ananoa kisu, anatafuta kondoo mwenye manyoya laini anamshika anamnyoa kondoo Yule na kwasababu hakuwa na uzoefu wa kunyoa kwani ulikuwa ni mpango wa dharula, kondoo alipiga kelele kwa maumivu na Isaka aliekuwa haoni kwasababu ya uzee, alijaribu kuuliza akiwa chumbani “jamanii huyo kondoo ana ninii? Mbona anapiga kelele?” na naweza kumuona Rebeka akimwonyesha Yakobo ishara ya kumwambia Shiii akiweka kidole kilicho wima mbele ya mdomo na kasha Rebeka kujibu mwenyewe” hakuna kitu baba alikuwa anataka kuingia jikoni nikamzuia eeh baba usiwe na wasi” haya yote ni ili amtengeneze Yakobo kuwa na manyoya kama Esau ili wamwingize kingi Isaka ambariki Yakobo badala ya Esau na mpango huu ulifanikiwa.



Tatu,Moja ya watu waliolelewa wakijijua wao ni nani na wapo Duniani kwa ajili gani ni Samson mtoto wa Manoa aliekuwa na nguvu nyingi kuliko mwanadamu yeyote alikuwepo Duniani,Inaamika angekuwepo leo angeweza kuzuia Treni isiondoke hata kama Dreva angeweka gia kiasi gani lakini alikwama kwa Delila,Delila anajua alivyomperemba na kumrubuni mpaka Samsoni akaingia kingi na kujikuta anapoteza unadhiri wa Mungu.



Nne, wanawake wengi waliondani ya ndoa watapotea na dhambi hii ya udanganyifu, unajua mwanaume kama ana mtoto nje ya ndoa huwa anakuwa mwepesi kumwambia mwenzake kwamba mpenzi unihurumie mwenzako nina mtoto kijijini na labda hili uliewe na mama anaitikia sawa nimekuelewa lakini wanawake wamekuwa wadanganyifu kwa wanaume hawako tayari kabisa kumwamia mumewe huyu mtoto sio wako hii mimba niliipata ulipokuwa safari na wanaume wengi wamelea watoto wakidhani ni wao wenyewe na wanapowakumbatia mama anaumia moyoni tu ooh maskini angejua! Lakini katu hayuko tayari kumwambia mumewe ukweli, ninyi ni mashahidi kwamba ktk wanandoa kumi wanaokwenda kupima watoto DNA kwa mkemia mkuu wa serikali,walau wanandoa watatu tu ndio wanatoka huku wakifurahi lakini saba kila mtu anatoka na mlango wake huku mwanaume akiongea mwenyewe kama kichaa na mwanamke akitoka huku ameangalia chini.



Mifano ni mingi inayoonyesha uwezo wa mwanamke kumdanganya mwanaume,sasa kwasababu mtoa mada alitangulia kusema, ni kubadilishana mawazo na hakuna atakaekasirika hili limenipa faraja na niseme kwamba wanawake wako juu ktk kudanganya kuliko wanaume

Reply to This

Wanawake

Reply to This

Reply to This

RSS

About

Bab Kubwa Media Bab Kubwa Media created this social network on Ning.

Tovuti bora. Sikiliza mziki wa Bongo popote Ulipo. Pata ladha ya Bongo. Chat, Photos, Videos & The latest and greatest Bongo Flava. Enjoy!



Forum

KAKANANII

ETI JAMANI KWANINI BONGO HAIENDELEI 9 Replies

Started by KAKANANII in General. Last reply by jojo Nov 19.

Zulekha

Walimu kuchapwa viboko 12 Replies

Started by Zulekha in General. Last reply by jojo Nov 19.

raul

mke wa mtu mtamu! 3 Replies

Started by raul in General. Last reply by njikalia mrema Nov 19.

Ummussalaam

Who Cheats More? Men or Women 6 Replies

Started by Ummussalaam in General. Last reply by jayjoe shoo Nov 18.

Said de Markson

UNDUGU MUHIMU

Started by Said de Markson in General Nov 6.

john bart

what a man got to do now:? 5 Replies

Started by john bart in General. Last reply by sarah ibrahim Oct 29.

raul

mama wa kambo 1 3 Replies

Started by raul in General. Last reply by jojo Oct 17.

mathias makunguru

ngono ya jinsia moja siyo.

Started by mathias makunguru in General Oct 13.

Ellinaza A.Killonzo

BBA REVOLUTION

Started by Ellinaza A.Killonzo in General Oct 10.

raul

mama wa kambo 2

Started by raul in General Sep 30.

mick john

KUFULIA C ISHU

Started by mick john in General Sep 25.

Boscow M. Maiso

Tanzanians Life 1 Reply

Started by Boscow M. Maiso in General. Last reply by Bab Kubwa Media Sep 12.

samson justo

nothing than lov

Started by samson justo in Lonely Hearts! Sep 11.

john bart

we can do it

Started by john bart in General Aug 31.

Hussein

wuold like to get to know u 4 Replies

Started by Hussein in Lonely Hearts!. Last reply by Hussein Aug 14.

yusuf mohammed khiranga lumumba

Hapo Cha Cha!!!!!!!!!!!!!

Started by yusuf mohammed khiranga lumumba in General Aug 13.

Robert frank mawalla

Hi.

Started by Robert frank mawalla in General Aug 9.

jmo

jmo

Started by jmo in General Aug 1.

© 2009   Created by Bab Kubwa Media on Ning.   Create Your Own Social Network

Badges  |  Report an Issue  |  Privacy  |  Terms of Service

Sign in to chat!