Bab Kubwa

Hapa nilipo umeme na maji uwa hayakatiki, hamna vumbi wala harufu ya dampo. Wapi kwingine kwenye sifa kama izo kama sio Ulaya? Naona nazidi kukuchanganya acha nikulaisishie niko UBALOZI wa MAREKANI. Nikikuambia nina bahati huezi kunielewa mpaka uone umati wa watu nje. Wote wamekatwa bogi wameambiwa wajaribu siku nyingine. Niko kamili na mabegi yangu mgongoni. Yani wakinigongea viza tu nawahi uwanja wa ndege.

Wazo la kwenda kutalii nje limenijia jana tu na ghafla nikajiuliza ikiwa wazungu wanakuja afrika kutalii kwa nini na sisi hatuendi kwao kutalii? Unaambiwa swali lilinisumbua mpaka ninamua leo nidamkie hapa ubalozini. Unajua hakuna hata mswahili mmoja anayekwenda sijui Serengeti, sijui manyara au mikumi eti kwenda kuangalia wanyama tumekuwa tukilala na mbuzi na ng`ombe. Kila siku tunakoswakoswa na fisi tukienda kisimani. Ivi tofauti ya swala na mbuzi ninayemchunga kila siku ni ipi?

Ane wei tusipoteze muda kwa blah blah. Nipo chumba cha mahojiano ya VISA. Tupo watahiniwa kumi hivi wote ukituangalia ni mashujaa, makomandoo. Wakati nimekaa hapo kijana akitokea dirisha la mahojiano akilia machozi kama mtoto mdogo. Sikutaka kujua nini kinamsumbua maana bongo matatizo mengi labda kapata habari za msiba au katumiwa majibu ya ukimwi kwa njia ya meseji.ntajuaje!.

“Zumbukuku Saidi” mwanaume nikajizoa zoa mabegi yangu na kuelekea dirishani huku roho ikinidunda. Hofu kubwa ni kimombo. Sijui hata cha kuombea maji. Dirishani mzungu anyeidhinisha viza akawa ameshajua tatizo langu. “mambo vipi mshikaji” jamaa akanisalimia “poa” nikampa kumbe jamaa Kiswahili anakijua kuliko hata mimi. Kakaa miaka 10 halafu maneno ya mtaani kafundishwa na nyumba ndogo yake ya manzese.

“Marekani unaenda kufanya nini?” Mzungu akaniuliza “kutalii”nikajibu kwa kujiamini. “Marekani hakuna wanyama wala mbuga, unaenda kutalii nini”? sitaki kuona wanyama wala mbuga nataka kuona mahali yalipolipuliwa maghorofa kwa ndege. Nataka kwenda kumuona shwaziniga na Rambo wanapoishi na kutembelea kiwanda cha fubu.

Benk stement unayo? Mmarekani akaoji. Ni nini hiyo? Nikauliza… una shilingi ngapi” mzungu akaona anirahisishie. Kwa mazoea ya ya wabongo nikajua mzungu anataka kunitoa upepo! “Hatuwezi kukupa visa kabla hatujajua una uwezo wa kujigharamia huko uendako” nimejiandaa vya kutosha mbali na tiketi ya kwenda na kurudi nina dola mia mbili” Zumbukuku laki nne ni pesa ya kulala na kula hotelini siku moja tu hotelini. “mheshimiwa mimi ntakula kwa mamantilie na kulala kwa washikaji” hiyo ni mbaya kwa uchumi wan chi mtalii anapaswa kuinua uchumi wa taifa sio kubana matumizi kwa kula na kulala kwa washikaji. “ah mbona hapa kuna watalii wa kizungu wanashindia madafu na kulala vichochoroni” nikaona mzungu ameosa la kusema “ una ndugu marekani?” sina

Zumbukuku tutaakikishaje kama utaludi? “jamani tiketi ya kurudisi hii nnayo” TIKETI SIYO KITU WATANZANIA MMEZOEAKUZAMIA KUTAFUTA MAISHA BORA ULAYA. “wanaozamia ni wale ambao hawasomi magazeti na kusikiliza habari. Rahisi kikwete ameahidi maisha bora kwa kila mtanzania. Nikimbie maisha bora nimwachie nani?

Ghafla nikaona ananyanyua mhuri mkubwa na kuigonga passport yangu, roho ikatulia kwamba hatimaye pamoja na kuniweka kitimoto hatimaye ananipa VISA! Akaingiza pasi yangu kwenye shimo la dirisha nikaichukua huku nikitabasamu. “Tutaonana” akaniambia.
Kwani na wewe unakuja marekani? Nikamwuliza. “Hapana tutaonana manzese”

Kuangalia pass yangu vizuri nikagundua kuwa kanigongea mhuri wa kuninyima viza. “ Maombi yako yanatia mashaka sijapata kusikia mtalii anaenda kuona maghorofa. TEMBELEA MIKUMI UJIVUNIE UTAIFA KAKA.

KA IYO NDUGU YANGU NIMEBADILI KAMPENI, “TWENDENI TUKATALII BONGO”

Share

Reply to This

Replies to This Discussion

Unajua jamaa inaonyesha alikua ajatulia kabisa.Ata kama unaela za kumwaga uwezi kuomba VISA ya kwenda USA kuangalia vitu kama hivyo.Itakua jamaa alikua mzamiaji tu ana lolote.Yaani ananikumbusha jamaa yangu mmoja wakati Marekani wanataka kuwachuku chura wa bwawa la Kiansi (wale chura wanaoweza kutoa nguvu za umeme) kwaajiri ya majiribio uko Marekani.Jamaa yangu akasema du maisha haya afadhari na mimi ningezaliwa chura wa Kiansi ningeenda Marekani.Bab kubwa maisha ndani ya Bongo yanawezekana tu,sio mpaka ugenini.

Reply to This

Nipo pamoja na Kenny. Maisha popote na mafanikio popote haswa ukiwa mwekujituma na bahati.

Reply to This

This is too funny,
Bro you made my day.

Reply to This

Mhh!!! ndugu yangu huyo alikuwa siyo mtalii ni mzamiaji, anataka kwenda ulaya akalale kwa washkaji na kula kwa mama ntilie, hilo pato la taifa watalipataje? Siku zote me naamini ukiwa mtu wa kujituma na muhangaikaji hakuna nchi yenye maisha bora kama Tz. Wale wenye kupenda kazi laini laini ndo utakuta kila siku wanawaza kukwea mchuma waondoke mnaondoka kwenda wapi msikae kwenye nchi yenu?

Reply to This

hiyo swa ni smart!nyc note..........tru dat!kwote mtaenda lakini hme ndiyo best

Reply to This

Jamaa akajua kwa kupiga deal atazamia. lol wakamtema bwana.
M x

Reply to This

ebwana kusema ukweli huyu jamaa nimemkubali sana, ni ukweli lakini, nani kasema ulaya watu wanakwenda kuangalia wanyama?
ulaya watu wanakwenda kushangaa majengo, magorofa, treni za umeme, watu maarufu, new places nsuch a thing mshkaji kawa mkweli sana tena sana. kama nataka kwenda kuangalia wanyama si angeenda mikumi tuu...
hawa jamaa wanatunyanyasa sana we acha tuu. ila jamaa kaaribu kwenye pesa ndogo sana mfukoni. n kila siku
wakati niko bongo nlkuwaga naona wazungu wanazurura na mabegi yao mjini wanapolala hatujui. labda gesti, au kwa washkaji nani anajua....

Reply to This

Reply to This

RSS

About

Bab Kubwa Media Bab Kubwa Media created this social network on Ning.

Tovuti bora. Sikiliza mziki wa Bongo popote Ulipo. Pata ladha ya Bongo. Chat, Photos, Videos & The latest and greatest Bongo Flava. Enjoy!



Forum

Ghaya

Love

Started by Ghaya in General 7 hours ago.

Ummussalaam

Who Cheats More? Men or Women 14 Replies

Started by Ummussalaam in General. Last reply by Ghaya 9 hours ago.

KAKANANII

ETI JAMANI KWANINI BONGO HAIENDELEI 11 Replies

Started by KAKANANII in General. Last reply by Arnold K. T. K. Dec 7.

Zulekha

Walimu kuchapwa viboko 12 Replies

Started by Zulekha in General. Last reply by jojo Nov 19.

Said de Markson

UNDUGU MUHIMU

Started by Said de Markson in General Nov 6.

john bart

what a man got to do now:? 5 Replies

Started by john bart in General. Last reply by sarah ibrahim Oct 29.

mathias makunguru

ngono ya jinsia moja siyo.

Started by mathias makunguru in General Oct 13.

Ellinaza A.Killonzo

BBA REVOLUTION

Started by Ellinaza A.Killonzo in General Oct 10.

raul

mama wa kambo 2

Started by raul in General Sep 30.

mick john

KUFULIA C ISHU

Started by mick john in General Sep 25.

Boscow M. Maiso

Tanzanians Life 1 Reply

Started by Boscow M. Maiso in General. Last reply by Bab Kubwa Media Sep 12.

samson justo

nothing than lov

Started by samson justo in Lonely Hearts! Sep 11.

john bart

we can do it

Started by john bart in General Aug 31.

Hussein

wuold like to get to know u 4 Replies

Started by Hussein in Lonely Hearts!. Last reply by Hussein Aug 14.

yusuf mohammed khiranga lumumba

Hapo Cha Cha!!!!!!!!!!!!!

Started by yusuf mohammed khiranga lumumba in General Aug 13.

Robert frank mawalla

Hi.

Started by Robert frank mawalla in General Aug 9.

jmo

jmo

Started by jmo in General Aug 1.

raul

kitendawili mapenzi

Started by raul in General Jul 17.

© 2009   Created by Bab Kubwa Media on Ning.   Create Your Own Social Network

Badges  |  Report an Issue  |  Privacy  |  Terms of Service

Sign in to chat!