Bab Kubwa

ni kisa kizuri chenye kuvutia kilicho mkuta kijana lamek na mama yake wa kambo baada ya kuachika mama yake mzazi ungana namimi usikose kisa hiki kifupi chenye kuhuzunisha na kufurahisha

MAMA WA KAMBO.

Nilikuwa nina miaka 25 pindi baba alipoamua kuoa baadaya kuachana na mama yangu mzazi ilipita kama miaka 5 tokea baba na mama walipotengana,baba na mama walitengana kutokana na sababu za kiwivu kwani mama alikuwa anamuona baba sio muaminifu katika ndoa yake.ndipo akaomba talaka kwenda kuishi na mama yake yaani bibi yangu kijijini,

Mama alipoachika baba hakutaka kuleta mke mwingne muda wote huo wa miaka mitano lakini baadaye nilistukia baba ananiita chumbani na kunambia ( lamek nafikiri umeshakuwa mkubwa si mtoto wa kufichwa kitu niliamua kukaa miaka yote hii bila kuleta mke nikifikiri kuwa mama yako anaweza kusahau yaliyopita na kurudi nyumbani lakini kama unavyoona njia zote nimejaribu ili aweze kurudi lakini imeshindikana)

Sasa keshokutwa anakuja mama yako mpya naomba uishi naye vizuri tu na muheshimu na kumuona kama mama yako mzazi) sikuwa na lakusema kwani ni haki yake mzee kuoa angalau moyni sikupenda kuona baba analeta mke mwingie humo ndani nilimjibu ( haina shida mzee lakini kipindi atakapokuja hapa waonaje kama nitaenda kuishi kwa babu mzee samba kwa muda wa miezi kadhaa then nitarudi)

Hapana lamek sikufichi sipendi uishi popote ple maadamu baba yako niko hai kwani hata mama yako alitaka kukuchuku lakini nimemkataza sasa akiona umeenda kuishi kwingine ataona nimemkataza makusudi samahani ana kwa hilo mwanangu naomba uwepo hapahapa paka hapo utakapofanikiwa maisha yako mwenyewe nakuweza kuishi peke yako) alinijibu mzee.

Sikuona sababu ya kumbishia mzee nilinyanyuka nakutoka nakuelekea chumbani kwangu, nikifikiria hivi kweli nitaweza kuishi na mama wa kambo maana nasikia mara nyingi hawapendi kuishi na watoto wakufiikia, { hodi,hodi,hodi) lamek!!1! nani!!? Nimimi Kelvin ok nisubiri nakuja alikuwa rafiki yangu Kelvin tuliyekuwa tunasma shule moja,

Ahaa muheshimiwa habari yako?, safi vipi wewe ? salama tu hivyo ndio kwanza natoka kuongea na mzee hapa nilikuwa naenda kujipumzisha bora umekuja maana usingizi hauji kabisaa} { vipi tena baba anataka uhame nini maana wazee wakishakuona umefikia balehe wanaanza kukukalisha vikao vya kukufukuza kijanja nyumbani}.

hapana si bora hata angenikubalia nihame kidogo ningeona nafuu lakini hilo kwa mzee gumu sana hata sijui nifanyeje maana hataki kabisa kusikia nahama, hapa nimejaribu kumgusia sasa hivi wakati tunaongea hataki kabisa kusikia nataka kuhama},

Sasa anataka nini mzee?, anataka amlete mama wakambo hivyo alikuwa ananipasha, nilitaka nikapumzike kwa mzee simba angalau mwezi tu wakati mama huyo anakuja hapa lakini kanikatalia kabisa,sasa si unajua mama wa kambo walivyo asije kuniletea Kosovo na mzee bure},

Aaaaaaah mzee anataka kuleta mama, kumbe itakuwa powa fujo za jikoni zitapungua,omba mungu tu mama awe mtu powa lakini akiwa freshfresh utaiona joto ya jiwe,kawaida lakini,si unajua mzee atakuwa ameshachoka kuishi pekee yake,sasa lamek sikiliza nimekuja hapa nina ujumbe wako,

leo chuoni wakati tunatoka nilkutana na pili amenipa ujumbe kuwa anaweza kuja home anahitaji uwepo anajambo muhimu sana anataka kukueleza sasa kama utakuwa na wakati itakubidi uje muheshimiwa, duh sidhani kama nitakuwa na muda huo kelvin maana kama unavyoona mzee naye leo karudi mapema},

inakubidi utafute njia yoyote ya kumwambia mzee maana kanisisitizia sana kasema usikose sasa usipotokea atatuona wakuja lamek, ok nitaangalia kama nitaweza mtomgoza mzee.

pili ni msichana ambaye nimetokea kumpenda toka mwaka wa kwanza chuoni mzumbe, nilipata tabu sana ya kumlubuni ili awe rafiki yangu kimapenzi, kwani ilinibidi nitumie njia mbalimbali ili niweze kufanikiwa, nilipoanza sikumuhitaji moja kwa moja awe mpenzi wangu bali nilimuomba tuwe marafiki ili tuweze kusaidiana katika masomo ya darasani,

Nilichukua mwaka na nusu hadi kumdhihirishia kuwa nampenda, na nahitaji awe rafiki yangu ikibidi tuje tufunge ndoa kabisa hapo baadaye,na nilimwambia kuwa kwa sababu nimeamua kumwambia bayana sitopendelea tusoma pamoja naye tena kama ombi langu atalikatalia kwani sababu ya mimi kusoma nayeye nikusubiria siku hiyo,

Jibu alilonipa nimpe miezi mitatu afikirie kama mimi nilivyochukua mwaka na nusu kwa kumwambia hayo, niliona mingi sababu alikuwa tayari keshajua dhamira yangu ,nilimjibu subiri nikafikirie ningemjibu kesho yake ,lakini usiku wa ile siku alinipigia simu huku akilia nakunambia,

Lamek sijui nikufananishe na nani au nikuiteje nashindwa kuelewa, mwakana nusu wote huo ulikuwa unafanya nini ukashindwa kunambia kuwa unanipenda, umenisababisha nitambue waganga na washauri wamapenzi kwa jili yako,

umesababisha nionekana mshamba wa mapenzi kwa rafiki zangu wa kike kwa kukataa wanaume wengine kwa ajli yako, umenifanya hata nikatae kusoma na marafiki zangu wa kike na kuniona kuwa naringa kwa ajili yako,

Kwanini hukuweza kuligundua hilo mapema na ukaweza kunambia na nikaepukana na kinyongo na mwiba ulionikaa moyoni kwa kufikiri vipi nitakupata wewe, lamek umenisababishia matatizo hata mama kunilaumu kila siku nikutajapo ananisema na kunambia kuwa kamwe hutoweza kutamka tena sababu imeshapita mwaka bila athari yoyote na kunitaka nikusahau,

Yawezekana ilikuwa ni kitendawili kati yetu alikuwa anatafutwa mteguaji, tambua lamek nilikuwa kwa ajili yako tokea hapo mwanzo ata mimi kukubali kusoma na wewe sikwa ajili eti siyamudu masomo, au sina wa kusoma naye au kwa ajili ya kusaidana la hasha, ni kwa sababu tokea siku nilipokuona nilipoingia shule nilishindwa kufikiria rafiki yeyote wa kiume tofauti na wewe,

Na nilikuwa nikiona kijana yoyote yule wa kiume nilikuwa naileta sura yako na kusema haiwezekani maadamu tunasoma pamoja lazima nijaribu, nakukumbusha kisa kimoja mimi na wewe katika mwaka wa kwanza shuleni tulipoingia baada ya miezi mitano nilikukuta kwa mwalimu elizah ofisini nikakuomba usiondoke unisubiri nina ujumbe wako,

Siku hiyo nilitaka kujaribu kukwambia lakini hukunipa nafasi,ndio kwanza uliongea wewe paka nikasahau kama nilikuwa na ujumbe, na uliponiuliza nikakwambia waonaje tubadilishe sehemu ya kujisomea twende darasa la mwaka wa nne, tokea siku hiyo paka leo hii bado tunasoma huko, siku ile huo haukuwa ujumbe isipokuwa nilisema tu baada yakuona siwezi kumaliza kutokana na muda na nilkuwa na kuonea aibu pia,

Nakupenda lamek usifikirie lolote lakunijibu hapa nilipo sikula kwa furaha niliyonayo nimemwambia mama hata hakuamini angalau sina uhakika kama ulikusudia kuwa na mimi kivipi walasijali, maana hiyo ni hatua moja kuelekea mbele,sasa basi kama ulikuwa unanijaribu naomba tambua moyo wangu ulivyo siku zote hizo,

Nimeona nisikufiche nikwambie tu maadamu umenichokoza na kunianza mwenyewe kwahiyo tambua kuwa mimi pili sina shaka na ombi lako na nakuomba kuwa serouse ilituweze kufika hatua ya pili byee . nashukuru sana pili ilove you 2 bye. alikata simu

Nilijisemea ama kweli hakuna aifutae riziki aliyoipanga muumba, ama wacheleweshaji wapo, tokea kipidi hiko mimi na pili tulikuwa marafiki na paka sasa hiv tuna mwaka mmoja urafiki wetu ni wawazi kwao na kwa wengi ktk marafiki zetu isipokuwa nashindwa kumueleza mzee hilo saabu mara nyingi mzee ananiusia kuwa nisipende wanawake katika kipindi cha masomo kwani wanake ni adui wa masomo,

Na hunambia elimu pekee ndio njia ya kumpata mwanamke ninayemtaka kwani nitapata kazi nzuri na na kuheshimika,{hello lamek mimi natoka naweza kuchelewa kurudi kuna masala nayafatilia kidogo uwanja ndege kija mtu yoote mwambie anitafute kesho au apige simu, ok sasa chakula nipike kngi au hapana usiniwekee pika kula tu,niliona kama zali wakati mzee ananiaga nipo na Kelvin tunafikiria jinsi ya kumtoroka nakumuaga mzee ilinikakutane na pili,

Aona hapa hakuna tena kizuwizi na kama ikiwezekana nitamleta hapahapa jiandaye tu na mzingira na kwasababu ni chakula cha peke yako unaweza kuika chakula cha watu watatu sawa muheshimiwa nadhani pili atafurahi sana siku ya leo kwa kukanyaga hapa kwenu,

Sasa unafikiri tupike nini bingwa maana
Tusije kuoekana wakuja kisha wengine hatujawahi kukaribisha mgeni hatujui wanaandaliwa nini, sikilza lamek kwani hata sikumoja hujawahi muuliza katika vyakula anapendelea nni? (ok ngoja nikaangalie kwenye kitabu changu cha kumbukumbu nitakuambia kwani nina notbook yake special) nikanyuka na kingia ndani kuchukua kitabu, njo na juie basi maana ninakiwi hapa alisema Kelvin.

Ok huyu jamaa bwana anapendelea makorona ya nazi yaliyochanganywa na nyama ya ngombe pia uji wa unga wa mtama uliochangaywa na maziwa ok hivi vyote niliwahi kupika, aliponiambia tu nikajiandaa na siku kama yaleo, saa basi wewe hutakiwi kuondoka kelvin ngoja tusaidiane hapa twende sokoni tukachukue nazi, makorona na nyama vipo.

Tulitoka kuelekea sokoni tukachukua vitu hivyo na kurudi, tuliviandaa sote kwa pamoja nakuitayarisha, kelvin aliniacha na kwenda kumsubiri pili niliipamba sebule kama vile ninasherehe ya birthday yangu,

nikapafusha udi wa manukato kisha nikakumbuka kuna haja ya zawadi niliwahi kwenda mjini na kuchukua saa ya kike ya mkononi mkufu na erenii zake za dhahabu na pete ya shaba yenye jiwe jekundu,kisha haraka nikachukua tax na kurudi home kuvihifadhi

Muda ulibakia kama nusu saa ivi wakina Kelvin kuja, nikakumbka kuwa nimesahau karatasi za kufungia zawadi za pili, mara simu yangu ikalia nikapokea, "hallo shikamoo" "marhaba ujambo, vipi ulishakula chakula tayari?" "Hapana bado mzee lakini ndio najiandaa kula" ,

Ok mama yako mdogo anataka kukusalimia ongea naye, halo lamek hujambo! sijambo mama vipi hali! salama tu vipi masomo, naendelea vizuri tu, "nilimwambia baba yako uje naye lakini amenambia unamitihani karibu", "ndio mama baba amenambia kuwa keshokutwa utaweza kuwa hapa nasi",

"Yh lamek mungu akipenda" " kwani mko wapi sasa hivi" niliuliza "tuko mikumi na huenda tukaenda kilimanjaro arusha, baba yako leo hatorudi tunaweza rudi kesho jioni mtu yeyote akija leo mwambie ampigie simu au aje kesho jioni"

"Ok mama nashukuru kwakunipigia simu" , "haya bye lamek" "bye mma", alikata simu. niliona kama zali sikuhiyo kwanza kuja kwa pili kisha mzee kutokurudi nyumbani ama kweli mungu ananipenda lazima pili alale hapahapa leo, sikuona haja ya kufata karatasi za kufungia zawadi kwanza muda ulikuwa umeisha,

Hodi!hodi! karibuni vipi mbona peke yako Kelvin, pili amekataa kuja huku amesema siku zote hutaki aje iweje leo umwambie aje!, "aaaakh Kelvin umeshindwa kumridhisha na kumwambia mzee hayupo sasa yuko wapi kwako hakuna amm", …hii ,,,hi pili, "angalia sasa Kelvin ulitaka kuniliza bure karibu ..kelvn napili walikuwa wanamtania lamek.

Pili nawe umekosea ungeacha kwanza tumyayushe hadi awe uji kabisa, "no naogopa asije kuzimia bure nikamkosa wakati bado hajanisha hamu" " haya karibun ndani lakini siku nyingine msifanye hivyo mnaweza kuwapeleka hospitalini wagonjwa wa presha"

Tukasalimiana na kuulizana hali nikanyanyuka ili nitenge vinywaji, "hapana mheshimiwa hutakiwi kunyanyuka hapo ulipo isipokuwa kama waelekea kusaini mkataba", "hapana nahisi koo pili limemkauka", "nipe idhini ya kujisevia nitakacho usije kujikwaa muheshmiwa pumzika"

Haya bwana Kelvin waweza ingia koote kasoro kwa mzee tu, "thnks muheshmiwa", Kelvin hakuleta juice tu alitandika meza na kuandaa msosi kamili tulikula nakufarahi hasa kizingatia chakula ndicho akipendacho mpenzi wangu pili,baada ya kumaliza kula na kupumzika Kelvin aliaga na kusema anatoka angerudi baada ya masaa mawili, "pili nakuomba usitoke hadi nirudipo nikupeleke nyumbani sawa?"

Sawa shemeji usihofu nakusubiri usichelewe sana tu unaju a tunakaa kwenye geti la mbwa mkali, "haina shida maadamu uko na mr hapo usihofu mbwa mwenyewe anatambua haki ya huyo mtu", "haya byee baadaye".

Sasa pili sikiliza leo mzee harudi amenipigia simu sasa hivi hapa nakunambia kuwa yuko mikumi na ataenda kilmanjaro, kesho jioni atarudi waonaje ukilala hapahapa leo mpenzi?.

Nini nilale hapahapa nyumbani nitasemaje then sijawahi kulala nje hata siku moja mama ataamini vipi kama nimelala kwako saingine umwambie wewe,

"Nimwambie mimi no dear watambua kuwa mimi kwenu sitambuliki rasmi, angalau ningekuwa mchumba nimekutolea barua tayari, hapo nusu aibu ingenitoka", "uoga wako tu mbona kwetu wanakutambua hatakama ujaleta barua, hasa mama ndio kabisa kwani anatambua jinsi ulivyokuwa unanipa tabu kipindi cha nyuma kabla hujasema kuwa unanitaka.

Sasa unanishauri vipi maana mimi leo sitaki kulala peke yangu kwenye jumba lote hili, "baba yako kaenda kikazi au kutembea tu?",aliuiza pili "no unajua baba keshokutwa anaoa sasa naona wameenda kutembea na mama mdogo mikumi na aliyenipigia simu mama akanambia kuwa baba leo harudi", "baba yako anataka kuoa?"

Ndio pili, baba amenambia hilo leo hii mchana kabla hajaondoka, sasa akisha kuja mama sidhani kama utaweza kuja hapa sitaki mama aelewe mambo yangu kwani baba mwenyewe mkali kinomi kwa masala ya mapenzi,

Sasa sikiliza lamek kama kweli baba yako anaoa kesho kutwa andika karatasi mualike mama kisha mwambie unaniomba nije huku leo kulala kusaidia kupanga vitu narudi kesho mengine niachie mwenyewe nitamalizia.

Ok ngoja nichukue karatasi basi, niliandika karatasi kama alivyotaka pili kisha nikampa na kumwambie aende numbani muda huo kwani akichelewa sana haitopedeza yawezekana kuna kazi home akazimalize, "haya mimi natoka tutaonana baadaye", "aaakh ngoja nimekumbuka kuna zawadi zako hapa mpenzi ngoja nikupe uende nazo".

Haya nipege maana moyo umeanza kuruka hapa kusikia hizo zawadi niliziweka kwenye bahasha na kuziweka kwenye mfuko, "angalia usizifungue na usimpe karatasi mama hadi uzione kwanza sawa?" "Sawa mpenzi sasa sisemi ahsante maana huenda sitozipenda byeeeee" aliania pili. ok alitoka pili .

Baada ya masaa mawili Kelvin alirudi, "vipi Lamek pili yuko wapi?" Amekwenda kuaga leo anakuajA kulala hapahapa" "unanitania muheshimiwa na mzee vipi"
'aaaaa sijakwambia mkuu amenipigia simu mama mdogo nimeongea naye mama anaonekana kijana maana hiyo sauti alafu simchezo, aonyesha kama ananijua maana ameongea kama aliwahi kuniona

Mhhhn sasa kama kijana tazama asije kukubambikia kesi na mzee ukimkatalia" "aaah namchoma kisu akiniletea za kuleta then naishia zangu nimeshachoka maisha na mzee ila basi huu mwaka uliobakia naona kama unachelewa.

Sasa mzee harudi leo pili amekubali kuja kulala hapa si unamjua hawezi kukataa ameenda kuaga mama yake kuwa anakuja kunisaidia kupanga vitu kwa ajili ya harusi ya baba keshokutwa", "duh lakini mama mwenyewe yule na muaminia hana kokolo wala matata". Alisema kelvin

Pili alipofika nyumbani alifungua zawadi yake na kukuta ni dhahabu, alifurahi sana akamuonyesha mama yake wote walifurahi, kisha akampa mama barua yake then akamwambia mama yake kuwa "lamek amenitaka nikalale kwake leo baba yake hayupo ameenda mikumi na mke wake huyo mpya watarudi kesho so amekuandikia hiyo barua alikuwa anaona aibu vipi nitaaga",

"Sawa kama unaenda huko angalia tu mwanangu uhakikishe kuwa anakuoa sioakufunue bure kisha kondom ni usalama kwako" "sawa hapana mama na kuhakikishia hatutofanya mapenzi niamini", "mhhn tumetokea hukohuko, {kitanda wanacholala wawili hakiachi kuimba}.

"Haya lakini mimi nakuhakikishia kuwa sitofanya lolote utakuja nambia, kama hujanipa zawadi" "haya nenda maadamu wajiamini ila uwahi kurudi usije kumletea mwenzako zahama na baba yake",

"Mama hata mimi nashangaa bado anamuogopa baba yake paka sasa hivi sijui itakuwaje, ananambia kuwa baba yake mkali kweli kwenye masala ya mapenzi sasa tunaweza kuoana tumalizapo shulekweli",

Usiwe na wasiwasi unalotakiwa umfanye lamek atambue kuwa yuko mkubwa na si mtu wa kupangiwa then utaona, kama anakupenda na hujawahi kumpa hata mara moja kweli atakuoa tu usiwe na shaka bint". Ok mama mimi naenda kesho haya byeeeeeeee.

Pili alirudii nyumbani kwakina Lamek huku akiwa mwenye furaha teeeeeele, then ilikuwa siku ya j/mosi siku ya j/pili hakuna shule, kwahiyo ilikwa siku muafaka kabisa, "hodi!hodi!" "karibu ohoo Kelvin! nimekutoroka nilijua nitawahi mimi unikute", "hunabudi nikuadhibu mimi nimewahi kurudi nimemuacha mke wangu huko analia nakuja huku nako haupo",

Aaaaaaaa pole ulivyotoka tu lamek akanifukuza akanambia ondoka hadi masaa mawili nirudi urudipo" "naona umetimiza ahadi", niliwakatisha maongezi "nilikwambia mama hana mashaka yuko mzungu anajali mtu mwenyewe ajue tu afanyalo, kisha ananiamini mtoto wake si mtu wa kukosea hovyo",

Ok karibu sana nyumbani kwa mzee mawazo, huenda unafungua mlango leo akija mama tu na sisi tunaweza toka kuangalia ustaarabu wetu, "huyo mama mwenyewe uliwahi muona?" "Hapana pili simjui lakini nahisi yeye amewahi niona kwani nimeongea naye leo anonekana ananifahamu kwani mtu asiyekutambua na anayekutambua kwenye maongezi utamuona tu".

"Angalia asije kuwa mama bora kwako na mtoto bora kwake" "kwanini unasema hivyo!? "ndio, maana mama bora hapendi mwanae kuishi mbali nayeye na mtoto bora hapendi kuishi mbali na mama yake", "sasa kuna ubaya hapo pili" "hakuna lakini panaweza kuzaa ubaya baaaye",

Muheshimiwa nafikiri hujamuelewa, shemeji pili anakusudia ukishakuwa bora kwake basi baba hawi bora tena, kama vile yeye akiwa bora kwako pili hatokuwa bora kwako,,,,"

"hilo haliwezekani kutokea pia ukizingatia huyo mama lazima atakuwa mkubwa sidhani kama ataweza kunizulia mas,ala mengine kama hayo,
siwezi fanya hivyo na nikiona ananiletea za kuleta naenda kwa babu mzee simba kuishi"

Hakika hatukubadilisha mazungumzo mengine isipokuwa tulimzungumzia mama wa kambo hadi Kelvin alipoaga na kutuacha nasi tukaingia ndani na kujipumzisha, lamek unakumbuka leo nilikuwa na ujumbe wa kukwambia jioni lakini kwasababu ulitaka nije nilale hapa sikutaka kusema ujumbe huo nafikiri huu ndio wakati muafaka, "ujumbe gani tena huo isiwe wataka nitoroka tu",

Hapana isipokuwa mama jana alinitaka nikuulize kulekule shule kuwa unafikiria nini kuhusu kuleta barua ya uchumba nyumbani", "barua?", " ndio mbona umestuka lamek kwani jambo geni hilo au hunampango wa kuja kunioa" "no ma dear pili hilo swala si tumekubaliana kuwa tukimaiza shule tutafanya hayo",

Unajua wakati huu mzee sidhani kama atanielewa nikimfikishia swala kama hilo, na miezi yenyewe imebaki michache, sasa siwezi kumwambia kitu kama hicho wakati jibu nalitambua pili, mimi nakuomba jaribu kumridhisha mama yako kuwa niko tayari kwa kila kitu na wewe walitambua hilo, isipokuwa hadi tumalize kwani atakuwa mzee hana sababu tena.

Angalau lengo la mzee nikumaliza shule nipate kazi ndipo nioe lakini kutoa barua haimaanishi kuoa, hana sababu ya kunizuwia hilo, nakuomba ongea na mama yako muonyeshe dhamira niliyonayo kuwa haina mapungufu yoyote, ili tuweze kumaliza siku hizi chache za msomo nimiezi sita tu sio mingi sana.

Ok nitajaribu vyovyte itakavyokuwa nitakujibu hofu ya mama anaogopa utakuja nikimbia baadaye na sina hoja,unatambua ninavyokupeda lamek sasa ukija nikimbia unaweza sababisha megine kwa upande wangu mpenzi,

hapana pili hayo sio mawazo kwasasa, waweza mfanya shetani akatawala mawazo yako na kuona naweza kukukimbia, hayo tusifikirie kwa muda huu tunachotaiwa sasa hivi ni kufikiria maisha ya pamoja si kufikiria uwezekano wa kukimbiana mpenzi mimi naogopa sana kitu hiko kutokea",

Ok nakuamini mpenzi mimi sina shaka na wewe, I promise you that I will be yours as am I jst now in a bed", "thnks mmwaah", tukazima taa nakulala paka asubuhii, pili aliogopa kukaa sana, saa tano aliondoka na kurudi nyumbani kwao, jioni baba alirudi na kukuta mazingira yamebadilka,

vipi jana ulikuwa na ugeni nini lamek?", "ndio mze alikuja kelvin na rafiki yangu tulilala sote", "aaaa ok", "sasa jiandae uende kwa shangazi zako na baba zako wakubwa kuwapa taarifa waambie kesho kuna harusi sitaki fujo hapa nyumbani, anayetaka kuja leo mimi nipo sitoki

Ok mzee nilivaa chapuchapu kisha nilitoka kumfata Kelvin anisindikize,tulitoa taariafa kwa watu kazaa ambao ni ndugu na majamaa, "kweli harusi hii ya kikubwa yani haina kadi wala karatasi" ,hakutaka tu mzee si unamjua mtu wa maaibu sana, ujumbe tuliopewa na baba kuwa kesho kutakuwa na magari hapo nyumbani saa nne kuelekea kihonda kumchukua bibi harusi,

Nilimshawishi Kelvin tuelekee hadi kihonda kupatazama kwa bibi harusi, tukachukua tax hadi kihonda tukatafuta nyumba yenye harusi hadi tukafika, kisha dereva wa tax akarudi sisi tukabakia huko sherehe iliyokuwa hapo si mchezo,

"mzee atawatia ndugu zake aibu sasa fujo yote hii nyumbani hakuna lolote itakuwaje hivi" wakati tuko tunashangaa pale na kuangalia wachezao mziki tuliitwa ndani na msichana tusiyemtambua lamek na mwenzako mnaitwa ndani,

Nani anatuita huyo sifahamu mimi nimeambiwa kuwa niwaite ndani kwa bibi harusi, tuliingia ndani nikijua kuwa hakuna mwinine isipokuw ni mma wa kambo, lakini ametutambua vipi wakati yuko chumbani, "twende Kelvin tutatambua hukohuko ndani",

Hodi! hodi! "piteni dani" " dah,mama salma!", "mama salma wee mtoto koma mama yako miye mhhn", "kweli hii ni surprise ya nguvu haya shikamoo mama" "marhaba ujambo" "sijambo za songea" " nzuri tu za mzumbe"

"safi haya imekuwaje kumnasa mzee mawazo kwenye nyavu hata mimi sielewi" "wewe mwenyewe ulikuwa hutaki kunifahamisha baba yako siku nyingi tu nakwambia nipe picha za ndugu zenu hutaki,

Sasa ndio hivyo yamewakuta" "sasa ulinijuaje mimi" " nimekujua juzi baba yako yuko kama wewe, maana siku zote hizo hataki kunileta kwenu namwambia anipe picha nimuone mke wake wa zamani hataki picha za mtoto wako hataki kaja kunipa juzi tayari tuko katika mipango ya harusi,

Nimeshindwa la kusema kang'ang'ania kuwa hawezi mwanawe kila siku kuingia jikoni na kuungua vidole wakati mimi nipo". Kelvin huyu ndio yule mama salma niliyokwambia miaka miwili iliyopita wakati tumekwenda iringa kutembea kishule,

Kisha wakaniacha na gari nikakwambia nilikua na mama mkarimu, alinikarimu vyooote ndiyo huyu, leo hii ni mama wa kambo sasa sijui itakuwaje,! au umepanga nini mama salma? "hakuna la kupanga hapa ni wewe mtoto mimi mama kwisha kazi kuna lingine la kupanga hapo tena",

inendelea

Share

Reply to This

Replies to This Discussion

nashukuru kuona maoni yako hii inanifanya nihisi wapo wasomaji kwa maoni yako unafikiri nini afanye huyu mtoto wakambo ili aepukane na msiba huu uliomkuta.

Reply to This

nashukuru kuona maoni unamshauri nini mtoto wa kambo hapo au ungekuwa wewe ungefanya nini

Flavia O Mgesi said:
pole sana kwa yote yaliyo kukuta.

Reply to This

mmh. inaendelea lini?

Reply to This

Reply to This

RSS

About

Bab Kubwa Media Bab Kubwa Media created this social network on Ning.

Tovuti bora. Sikiliza mziki wa Bongo popote Ulipo. Pata ladha ya Bongo. Chat, Photos, Videos & The latest and greatest Bongo Flava. Enjoy!



Forum

KAKANANII

ETI JAMANI KWANINI BONGO HAIENDELEI 9 Replies

Started by KAKANANII in General. Last reply by jojo Nov 19.

Zulekha

Walimu kuchapwa viboko 12 Replies

Started by Zulekha in General. Last reply by jojo Nov 19.

raul

mke wa mtu mtamu! 3 Replies

Started by raul in General. Last reply by njikalia mrema Nov 19.

Ummussalaam

Who Cheats More? Men or Women 6 Replies

Started by Ummussalaam in General. Last reply by jayjoe shoo Nov 18.

Said de Markson

UNDUGU MUHIMU

Started by Said de Markson in General Nov 6.

john bart

what a man got to do now:? 5 Replies

Started by john bart in General. Last reply by sarah ibrahim Oct 29.

raul

mama wa kambo 1 3 Replies

Started by raul in General. Last reply by jojo Oct 17.

mathias makunguru

ngono ya jinsia moja siyo.

Started by mathias makunguru in General Oct 13.

Ellinaza A.Killonzo

BBA REVOLUTION

Started by Ellinaza A.Killonzo in General Oct 10.

raul

mama wa kambo 2

Started by raul in General Sep 30.

mick john

KUFULIA C ISHU

Started by mick john in General Sep 25.

Boscow M. Maiso

Tanzanians Life 1 Reply

Started by Boscow M. Maiso in General. Last reply by Bab Kubwa Media Sep 12.

samson justo

nothing than lov

Started by samson justo in Lonely Hearts! Sep 11.

john bart

we can do it

Started by john bart in General Aug 31.

Hussein

wuold like to get to know u 4 Replies

Started by Hussein in Lonely Hearts!. Last reply by Hussein Aug 14.

yusuf mohammed khiranga lumumba

Hapo Cha Cha!!!!!!!!!!!!!

Started by yusuf mohammed khiranga lumumba in General Aug 13.

Robert frank mawalla

Hi.

Started by Robert frank mawalla in General Aug 9.

jmo

jmo

Started by jmo in General Aug 1.

© 2009   Created by Bab Kubwa Media on Ning.   Create Your Own Social Network

Badges  |  Report an Issue  |  Privacy  |  Terms of Service

Sign in to chat!